Breaking News

SERIKALI YAKABIDHI KWA MWANASHERIA MKUU KANUNI ZA KUPIGA MARUFUKU MIFUKO YA PLASTIKI.


Na Furaha John, Dodoma

OFISI ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, imekabidhi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanuni zitakazo tumika katika katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini zitakazotumika kishera ili aweze kuzipitia kabla ya kuanza kutumika rasmi.

Hatua hiyo imefikiwa muda mfupi baada ya tamko la Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kutangaza Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plasiti nchini ifikapo Juni 1, mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Januari Makamba wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya katazo hilo lililotolewa na serikali.

Makamba amesema maamuzi yaliyotolewa na Waziri mkuu juu ya matumizi ya mifuko hiyo siyo la kushitukiza kwani tayari seriklai ilishashirikisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali.

Amefafanua kuwa tayari kanuni zilikwisha andaliwa na juzi baada ya tamko la waziri mkuu, usiku huo huo wizara ilizikabidhi kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili azipitia na atakapozirejesha zitakuwa tayari kwa kuanza kutumika.

 “Tunachokifanya ni utekelezaji, kanuni tulikwishaziandaa na tumezikabidhi kwa mwanasheria, kuanzia ijumaa tutakuwa na vikao na wadau mbalimbali ili kuweka sawa sawa jambo hilo, mana si geni na wadau wote ikiwemo wamiliki wa viwanda wapo tayari,”amesema.

Waziri huyo ameeleza kuwa, kanuni hizo zitaeleza adhabu ambazo zitatumika wakati ambao mtu atabanikika kutengeza, kutumia au kusambaza mifuko hiyo iliyopigwa marufuku.

Amesema, kanuni hizo zimeweka adhabu kwa watengenezaji pamoja na watumiaji kulingana na kos,  pia zitaonyesha ni aina gani ya vifungashio havija pigwa marufuku na havitahusika katika kanuni hizo.

Makamba amevitaja  baadhi ya vifungashio vya plasitiki ambavyo havitapigwa marufuku ikiwemo katika dawa,vyakula kama vile maziwa ya Tanga fresh, pembejeo na mbegu zinazotumika katika kilimo, pamoja na chupa za plastiki ila kutakuwa na utaratibu maalum wa kuvikusanya.

Sambamba na hilo alisema kupitia  kanuni hizo kitaundiwa kikosi kazi cha kuzisimamia ambapo wajumbe wake watatoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Baraza la mazira la taifa (NEMC), Mamlaka ya mapato nchini (TRA), pamoja na Uhamiaji.

Wajumbe wengine ni Mamlaka ya usafiri wa anga (TAA), Shirika la viwango nchini (TBS), Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), Polisi, Wizara ya viwanda na biashara pamoja na taasisi zingine.

"Watu wa TAA wao watakuwa na jukumu la kutoa matangazo katika vyombo vyao vya usafiri wa anga kuwatanzania abiria kuwa wanapoingia katika viwanja vyetu vya ndege kutoka nchi nyingine wasije na mifuko ya plasitiki”alisema.

Amesema, serikali tayari imeshafanya utafiti na kujiridhisha kuwa upatikani wa mifuko mbadala ipo ya kutosha kwani tayari walishakutana na wazalishaji ambao walikuwa wanasubiri katazo la serikali ili kuanza kuzalisha kwa wingi.

Akizungumzia athari za viwanda vya ndaniamesema, asilimia 80 ya mifuko ya plastiki inayotumika hapa nchini inatoka nje ya nchi, wao wanatengeneza na kutupa takataka hizo Tanzania ambapo mfuko mmoja ukitupwa unachukua miaka 500 hadi kuoza kwake.

" Najua wapo watu watajitokeza na kutoa kauli mbalimbali kuhusu katazo hilo lakini wanaamini na wanaridhika kuwa hakutakuwa na hasara ila fulsa zitaongezeka kwa wale wanaojishughulisha na ufumaji wa mifuko mbadala ikiwemo vikapu kwa kutumia ukindu,"amesema.


No comments