Breaking News

WADAU, SERIKALI WAJADILI NAMNA YA KUDHIBITI RUSHWA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akiwasili Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Dr. Mary Mwanjelwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani na Naibu mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Kabudi (katikati) akiwa kwenye mkutano wa wadau kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi wa serikali za mita 2019. Kushoto kwa Prof Palamagamba John Kabudi ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dr. Mary Mwanjelwa,akifuatiwa na Naibu mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani,akifuatiawa na Mkurugenzi wa utafiti na ufuatiliaji wa TAKUKURU Sabina Seja.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba kwa wadau(hawapo pichani) kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Profesa Kabudi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliohudhuria warsha ya kujadili namna ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019. kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani, akifuatiawa na Mkurugenzi wa utafiti na ufuatiliaji wa TAKUKURU Sabina Seja na Mbunge wa Vunjo Mhe. James Mbatia. Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dr. Mary Mwanjelwa,akifuatiwa na Naibu mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo na Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza.

No comments