Breaking News

WANAFUNZI KAHAMA WATAKIWA KUZINGATIA VEMA MASOMO YAO.


KAIMU Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma Dk. Arnold Towo amewaeleza wanafunzi wa Kidato cha I hadi 6 wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kuzingatia  vema masomo yao ili kuwa na msingi bora wa elimu na kuweza kuchagua masomo yao vema ili kukidhi mahitaji yao wanapofikia hatua ya kujiunga katika Masomo ya Shahada za juu.

Amesema hayo wakati wa ziara fupi iliyofanywa na uongozi wa shule ya Mt. John Paul II pamoja na wanafunzi 55 walipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo na kufahamu utendaji kazi wa Chuo Kikuu Mlimani.

"Napenda kuwasisitiza wanafunzi kutumia muda wao vema wa masoma, kujituma na kujifunza vitu tofauti pamja na kutambua mapema kile unachotaka kusomea ili inapofika wakati wa kujiunga na chuo kikuu wawe wamejitambua na kufahamu vema wanataka kusoma nini, alisisitiza Towo.

Miongoni mwa vitu walivyojifunza wakati wa ziara ni pamoja na kufahamu taratibu na vigezo vya kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kutoka kurugenzi ya masomo ya Shahada ya awali, masuala ya uhandisi wa umeme na kupata kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya historia ya Afrika pamoja na kutembelea na kuona jinsi maktaba mpya inavyofanyakazi.

Ameongeza kuwa, kikubwa katika masomo wanafunzi wanatakiwa kuwa na ujuzi wa juu na ufaulu bora na wenye uwezo wa kujieleze ili kukidhi hitaji la soko pale wanapohitimu masomo yao ya juu.

"Lengo kuu la ziara hii kwa wanafunzi wetu ni kuwajengea uwezo na kuona kwa vitendo yale wanayosikia kuhusu chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa ya kujituma katika masomo pale wanaporejea shuleni", alisema Julius.

Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kinatoa huduma kuu tatu ambazo ni Kutoa Elimu, Kufanya Tafiti pamoja kutoa huduma za ushauri kwa Mashirika ya umma pamoja na Sekta binafsi.

No comments