Breaking News

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KUJADILIANA.

Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Doto James akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma .

Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji , (watatu kushoto) wakiimba wimbo wa kudumisha umoja kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma .

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa kudumisha umoja na mshikamano "solidarity forever"  kabla ya kuanza Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma .

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto) akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli na kuapishwa hivi karibuni , Adolf Ndunguru, katika Baraza la Wafanyakazi wa Wazara hiyo , Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Doto James akitoa salam za utangulizi kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani),  wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), katika ukumbi wa Kambarage Dodoma ambapo Watendaji wa Wizara walitakiwa kutekeleza jukumu la kugawa rasilimali fedha kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoainishwa kwenye Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa kufungua Baraza la Wafanyakazi, Jijini Dodoma, ambapo aliagiza Watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kuboresha mifumo ya kukusanya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa walipa kodi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akipongezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, baada ya kumaliza hotuba yake alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.

Meza Kuu (waliyokaa) ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji,(watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasilino Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments