Breaking News

BAADHI YA MATUKIO YALIYOTOKEA BUNGENI LEO MEI 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Bungeni jijini Dodoma Mei 28, 2019.
 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiteta na Naibu wa Waziri wake, Subira Mgalu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 28, 2019.
 
Dkt. Medard Kalemani akielekea kwenye eneo maalum la kusoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma, Mei 28, 2019.


Dkt. Kalemani akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake, Bungeni jijini Dodoma, Mei 28, 2019. 
 
Majaliwa akizungumza na Waziri wa Elimu ,Sayansi, Tekinolojina na  Ufundi, Profesa, Joyce Ndalichako, Bungeni jijini Dodoma, Mei 28, 2019.  
 
Mjaliwa akisalimiana na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 28, 2019. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  Dastan Kitandula akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo Bungeni mara bada ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Bungeni Jijini Dodoma.
 
Mbunge wa Muleba Kusini  Charles Mwijage akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020 leo Bungeni Jijini Dodoma.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)Mhandisi Amos Maganga nje ya viwanja vya Bunge leoJijini Dodoma.
 
Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi , Watendaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakifuatilia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.

Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa baadhi ya wageni waliofika Bungeni kwa lengo la kujifunza shughuli za Bunge mapema leo.
 
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha  kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya umeme .

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na FrankMvungi- MAELEZO)

No comments