Breaking News

DIWANI CHADEMA ATIMKIA CCM


Aliyekuwa Kada na Diwani wa viti maalum Wilaya ya Ubungo (CHADEMA) Liberata Samsoni amejiuzuru nafasi yake na kuhamia CCM kwakile alichokiita kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano.

Liberata kupitia barua rasmi aliyoiandika kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo amesema kuwa yuko tayari kutumikia na kuahirikiana na CCM katika sehemu yoyote ili kuwaletea wananchi maendeleo.

"Nimeridhishwa sana na kazi zinazotekelezwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kuwaletea Watanzania Maendeleo." Ameeleza Liberata.

Liberata amehudumu CHADEMA tangu mwaka 2016 katika nafasi ya Udiwani wa viti maalumu Wilaya ya Ubungo.

No comments