Breaking News

JPM ATENGUA UTEUZI WA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA WAWILI.Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe  Adelius Kazimbaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora HadijaMakuwani.

Dkt. Magufuli ametengua uteuzi wa Wakurugenzi hao kuanzia leo tarehe 16 Mei, 2019.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo katika kikao cha kazi kati yake na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, WakuuwaWilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wakurugenzi wa Halmashauri hizo watateuliwa baadaye.


No comments