Breaking News

LUKUVI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA BODI YA WAKURUGENZI NHC.WAZIRI WA ARDHI Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ameipa maagizo mazito Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo ameipa miezi mitatu ya kufanyia maamuzi maagizo yake.

Waziri Lukuvi ametoa maagizo hayo katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao wameteuliwa hivi karibuni hayo ameipa bodi hiyo mpya miezi mitatu ya kujifunza yale watakayoyasimamia kwani wengi wao wanatoka katika idara nyingine zisizo za NHC hivyo wapo huru kuchunguza idara yoyote na kama kuna mkurugenzi haoneshi ushirikiano wamlipoti na yeye atamchukulia hatua.

Mei 27 mwaka  huu Uteuzi huu umefanyika baada ya kuvunjwa kwa Bodi hiyo Mwaka 2017 ambapo Rais Dkt. John Magufuli alimteuwa Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Sophia Kongela kufuatiwa na baadae Lukuvi kumteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Maulid Banyani kukaimu nafasi hizo.

Wajumbe hao wapya ni pamoja na Sauda Msemo Kamishna Msaidizi Sera na Madeni Wizara ya Fedha na Mipango, Abdalla Mwinyimvua Mhasibu, Martin Madekwe Mstaafu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa na Charles Singili Mkurugenzi Mtendaji Benki ya (TIB).

Wengine ni Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi, Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mhandisi Mwita Rubirya ambapo kwa pamoja  atashirikiana na Mwenyekiti wa bodi  Dkt. Sophia Kongela pamoja na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Dkt. Maulid Banyani.

No comments