Breaking News

RAIS MAGUFULI AREJEA NCHINI KUTOKA NCHINI ZIMBABWE.Dkt. John Magufuli leo tarehe 30 Mei, 2019 amerejea hapa nchini akitokea nchini Zimbabwe ambako amefanya Ziara Rasmi ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya  Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.

Kabla ya kufanya ziara nchini Zimbabwe, Rais Magufuli amefanya ziara nchini Afrika Kusini ambako pamoja na kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Awamu  ya Tano wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefanya mazungumzo na kiongozi huyo, Ikulu Jijini Pretoria.

Baadaye,  Rais Magufuli akaelekea nchini Namibia ambako amefanya Ziara ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Dkt. Hage Geingob ambapo pamoja na kufanyanae mazungumzo alifungua mtaa mkubwa uliopatiwa jina la Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na pia alitembelea eneo walipozikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia na kiwanda cha nyama cha Meatco.

Alipo wasili katika uwanja wandege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,  Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo.
No comments