Breaking News

SERIKALI YAJIPAMBANUA KUPELEKA HUDUMA ZA AFYA BURE KWA WAJAWAZITO.


Na Furaha John, Dodoma.

SERIKALI  imesema takribani kinamama milioni 2 wanajifungua kila  mwaka hapa  nchini hivyo inaandaa sera ya matibabu bure kwa wajawazito kuanzia mimba mpaka kujifungua.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Dodoma leo na Naibu waziri wa Wizara hiyo, faustine Ndugulile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Kemilembe Lwota(CCM),ambaye alitaka kujua  lini  serikali itaona umuhimu wa kuchangia huduma za uzazi kwa  wakinamama wajawazito ili waweze kupatiwa vifaa na huduma  hiyo bure na kuondoa malalamiko yaliyopo.

Ndugulile amesema, serikali imekuwa ikitoa 
dawa  na vifaa  vya kujifungulia kwa  wakinamama wajawazito bure katika hospitali hapa nchini.

Kuhusu malalamiko naibu waziri amesema ni  sehemu ndogo ya malalamiko ndio wanayapata kuhusiana na upatikanaji wa vifaa hivyo na dawa.

Awali katika swali la msingi Mbunge wa Kaliua Magdalena Sakaya(CUF), alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza Kwa ukamilifu Sera ya Afya ya kutoa huduma za afya bure kwa wanawake wajawazito kuanzia siku ya kupata mimba mpaka atakapojifungua, Watoto chini ya miaka mitano pamoja na wazee wenye umri zaidi ya miaka 60.

“Mwaka 2014 serikali ilianza utaratibu wa kuwapatia wazee vitambulisho Kwa ajili ya matibabu bure kwenye  Zahanati, vituo vya afya na hospitali, je ni  Wilaya ngapi zimekamilisha utaratibu huu muhimu ili kuokoa maisha ya wazee yanayopotea kwa  kukosa huduma  za afya,” Alihoji Magdalena

Akijibu Ngudulile amesema, serikali imekuwa ikifanya jitihada katika kutoa huduma bora za afya na zenye kufikiwa na watu kwa  kuandaa Sera na miongozo na kusimamia utekelezaji wake.

No comments