Breaking News

UMMY MWALIMU AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Biashara kutoka Shirika la AFRIpads  Liz McNeil wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu akishika Taulo ya kike kuangalia ubora wake katika  maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mak’s Ama Home Pharmacy.

Waziri Ummy Mwalimu akisoma jarida la Fema wakati alipotembelea katika Banda lao katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma kushoto ni Msaidizi wa Masuala ya Kihabari kutoka Shirika la Femina Hip Sekela Mwaipaja.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa na wadau wa hedhi Salama wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma.

 Waziri Ummy Mwalimu akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya wadau wa Hedhi Salama nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
Picha na Wizara ya Afya


No comments