Breaking News

WAZIRI MKUCHIKA AFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIONGOZI WA WIZARA YA MADINI.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika  akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri Mkuchika (hayupopichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Waziri Mkuchika akikabidhi cheti cha ufanyakazi bora kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara ya Madini, Asteria Muhozya baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Bw. Issa Nchasi (kulia).

Waziri  Mkuchika na Waziri wa Madini, Doto Biteko wakifurahia jambo baada ya ufunguzi mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini  Issa Nchasi.


No comments