Breaking News

BAADHI YA MATUKIO YALIYOJITOKEZA KATIKA ZIARA YA PROF.KIKULA NAMUNGO.


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa kwanza kushoto na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wa pili kushoto, wakiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Nachingwea Rukia Muwango wa kwanza kulia na kulia kwake ni katibu tawala mkoa wa Lindi na Afisa madini mkazi mkoa wa Lindi kushoto kwa RC.


Prof. Kikula wa nne kulia na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wa tatu kushoto, wakiangalia na kukagua sampuli za miamba zilizohifadhiwa kwenye mifuko kutoka kwenye mwamba wa madini ya dhahabu kutoka mgodi wa Namungo.Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma akiwa chini ya shimo kwa ajili ya kuchukuaa vipimo kwenye mwamba uliochukuliwa sampuli na Madini ya Graphite kwenye eneo la kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd mara baada ya kutembelea eneo.


Fundi Sanifu Mwandamizi Paulo Shauri  wa kampuni ya Lindi Jumbo katikati akionyesha na kutoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula kulia kwake na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma kushoto kwake  kuhusu muundo na muonekano wake pindi utakapo anza kufanya kazi hapo mwakani mwezi August 2020.

No comments