Breaking News

DKT. KIGWANGALLA AKUTANA NA WANANCHI ALAITOLE NA KUTATUA MIGOGORO YAO.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Hata hivyo Waziri Kigwangalla ameumaliza mgogoro huo kwa kuagiza wakazi hao wapewe kibali cha ujenzi na mamlaka hiyo katika eneo lililopendekezwa.
                     
Dkt. Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maoni na hoja za wananchi wa Kata ya Alaitole alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  katika eneo lao la Esere, wilayani Ngorongoro jijini Arusha.   

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro William Ole Nasha akizungumza na wakazi wa Kata ya Alaitole iliyo ndani ya Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilizuiwa kujenga shule ya bweni ya wasichana na mamlaka hiyo zuio ambalo limeondolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii aliyefika katika kata hiyo kutatua mgogoro huo.

Dkt. Kigwangalla na wananchi wa Kata ya Alaitole katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.  Kigwangalla alifika kutatua mgogoro uliohusisha wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Dkt. Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kupitishwa na katika eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale ambalo bado taarifa zake zinaendelea kufanyiwa utafiti katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro.

Dkt. Kigwangalla akiwa ameambatana na  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro William Ole Nasha na askari wa uhifadhi wakiangalia eneo itakapojengwa shule ya wasichana ya bweni ya kata ya Alaitole.

Dkt. Kigwangalla, viongozi na wananchi wa Kata Alaitole wakitazama eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale lililogunduliwa na wakazi hao katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Taarifa kuhusu fuvu hilo zinaendelea kufanyiwa utafiti na watalaam.

Dkt. Kigwangalla akisalimiana kwa furaha na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro.  PICHA/ Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments