Breaking News

DKT. MWANJERWA ATEMBELEA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA KAMPASI YA TABORA.

Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) akiwasilisha ripoti ya chuo wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya UtumishiwaUmma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (kulia) na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kampasi ya Tabora.Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kampasi ya Tabora katika kikao kilichofanyika chuoni hapo mkoani Tabora. 


Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kampasi ya Tabora, Dkt. Ramadhan Marijani akijibu hoja za Dkt. Mary Mwanjelwa  (kushoto) wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri na watumishi wa chuo hicho.Dkt. Mary Mwanjelwa akichapa kwa mashine alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kampasi ya Tabora. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel Shindika (kushoto) na Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kampasi ya Tabora, Dkt. Ramadhan Marijani.


Dkt. Mary Mwanjelwa akikagua jengo jipya la ghorofa mbili la Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kampasi ya Tabora. Wengine ni Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora, Dkt. Ramadhan Marijani na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.

No comments