Breaking News

JPM AFIKA SOKONI FERRY WAKATI AKIFANYA MATEMBEZI LEO JIONI.

Dkt. John Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Samaki katika Soko la Samaki la Ferry kuhusu umuhimu wa kutumia mifuko mbadala na kuachana na kutumia mifuko ya plastiki wakati alipopita katika matembezi ya jioni.

Dkt. Magufuli akinunua samaki na kuwahifadhi katika kikapu chake cha kiasili wakati alipokuwa matembezini katika maeneo hayo ya Ferry.


Dkt. Magufuli akiangalia Samaki mbalimbali katika Soko la Ferry mara baada ya kufika eneo hilo.
Dkt. Magufuli akiwa amebeba samaki wake kwa kutumia Kikapu mara baada ya kuwanunua katika Soko la Samaki la Ferry jijini Dar es Salaam.


Dkt. Magufuli akikagua Samaki kabla ya kumnunua kutoka kwa mfanyabiashara wa Samaki Abraham Kaberege wakati alipkuwa katika matembezi ya jioni katika maeneo ya Soko hilo la Ferry jijini Dar es Salaam.

Dkt. Magufuli akinunua samaki huyo mara baada ya kumkagua.


Dkt. Magufuli akizungumza na wauza kahawa katika eneo la Soko la Ferry ambapo aliagiza kuboreshwa kwa sehemu ya biashara hiyo kuanzia siku ya kesho. PICHA NA IKULU.


No comments