Breaking News

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA LUCAS MALIA LINDI.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Agnes Venance (kulia) na Paskazi Mashimo (katikati) ambao alisoma nao katika Shule ya Msingi ya Mnacho wilayani Rungwa kwenye miaka ya 70 .  Alisalimiana na wanafunzi wenzake hao baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019.

                         Majaliwa na mkewe Mary wakisalimina na Watawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho baada ya Waziri Mkuu, kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019.


Majaliwa akizungumza na Paroko wa Parokia ya Mnacho, Padri Gerold Nyagau (wa pili kushoto) wakati alipokagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu David Mwakalobo. 


Majaliwa  akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Mnacho wilayani Ruangwa, Juni 2, 2019. Kushoto ni Mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu  David Mwakalobo.


Majaliwa  na Paroko wa Parokia ya Mnacho wilayani Ruangwa, Padri Gerold Nyagau wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza baada ya Ibada ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Mnacho, Juni 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


No comments