Breaking News

MWALIMU MKUU AMPA MIMBA MWANAFUNZI DARASA LA SABA.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Nyantole, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, amelazimika kukatisha masomo yake baada ya kupata ujauzito, unaodaiwa kuwa ni wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo  Jackson Rwekaza .

Akisimulia chanzo cha kupata ujauzito huo jana nyumbani kwao mwanafunzi huyo mwenye miaka 16, alikiri kuwa na mahusiano na mwalimu Rwekaza ,kwa kipindi cha miezi mitano ambapo alimshawishi na kukutana nae kimwili na kupelekea kupata  ujauzito.

Alisema wakiwa shuleni hapo mwalimu wake alimuomba waendo sokoni Mwanga na baada ya kufika alimnunulia sketi ya shule na baada ya hapo alimuomba amsindikize nyumbani kwa mama yake ndipo alipompeleka nyumbani kwake na kumuingilia kimwili ndipo ikawa chanzo cha uhusiano wao.

Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa anaishi kwa Bibi yake Katika Kijiji cha Mwandiga, anasema baada ya kuendelea na uhusiano huo alijikuta amepata ujauzito na baada ya kumwambia mwalimu huyo alimuomba atoe mimba hiyo na baada ya kukataa kutoa alikata mawasiliano nae.

" walikuja kupima mimba shuleni nikawa nimemwambia na mimi nipime akaniambia niseme kwamba sina mkojo ilinisipimwe lakini nilikuwa mjamzito, kwa sasa naona aibu kwenda shuleni kwa kuwa wenzangu watanicheka na hata mwalimu mwenyewe hataki kupokea simu wala hataki nimuone tangu amenipa hii mimba", alisema mtoto huyo.

Hata hivyo Mama mzazi wa mtoto huyo Sakina Kazili, alieleza kusikitishwa na kitendo hicho na kuomba serikali kumchukulia hatua kali mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Jackson Rwekaza ili haki iweze kutendeka inavyostahili.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Pendo Mangali, alikiri ofisi yake kuwa na taarifa juu ya suala hilo na kwamba hatua za kiutumishi zimeanza kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Otieno, alisema mtuhumiwa alikamatwa na kuachiwa kwa dhamana  kwa kuwa uchunguzi ulikuwa bado haujakamilika .

Alisema baada ya uchunguzi kukami watahakikisha sheria inachukua mkondo wake na kukohakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kabisa.

 Pia kamanda Otieno ametoa onyo kwa walimu  na vijana wengine kuacha tabia za kuwa na mahusiano na wanafunzi, kwani wanawafanya  wanafunzi kupoteza ndoto zao na kwaatakae kamatwa ni lazima atafungwa miaka 30.

Kwa mujibu wa Ofisa elimu Mkoa wa Kigoma Juma Kaponda alisema kwa mwaka 2017/2018 jumla ya watoto 190 wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na kupata ujauzito wakiwa shuleni, mpaka sasa matukio hayo yanaendelea kutokana na wazazi wengi kutokuwa na muda wa kufuatilia mienendo ya watoto wao.

No comments