Breaking News

PROF. KABUDI AZUNGUMZA NA IDARA YA ITIFAKI YA WIZARA YAKE.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba  Kabudi kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara yake baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John  Magufuli, kwenye nafasi hiyo tarehe 3 Machi 2019. 

Pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi aliwataka Watumishi hao kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa kushirikiana na  kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 


Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje.

 Aidha, mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es Salaam tarehe 04 Juni, 2019 

No comments