Breaking News

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA BODI YA TTCL.Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Magufuli amemteua Mohammed Abdallah Mtonga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Mtonga anachukuwa nafasiya Dkt. Omari Rashid Nundu ambaye ameteuli wa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

Uteuzi wa Dkt. Omari Nundu katika nafasi hiyo unafuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania anapaswa kuteuliwa na Serikaliya Tanzania.

Kwamujibu wa makubaliano hayo Afisa Mkuu wa Ufundi (Chief Technical Officer – CTO) pia anateuliwa na Serikali ya Tanzania, na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt. Prosper  Mafole.

Wajumbe wengine watakaoiwakilisha Serikali katika Bodi ya Airtel Tanzania ni John Sausi na  Lekinyi  Mollel.
Uteuzi huu unaanza leo tarehe 12 Juni, 2019.


No comments