Breaking News

RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA NCHI NZIMA KESHO IJUMAA JUNE 07, 2019.
Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Magufuli keshotarehe 07Juni, 2019 atakutana na wafanyabiashara kutoka Wilaya zote hapa nchini na wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

Wafanyabiashara watano kutoka kila Wilaya hapa nchini watawawakilisha wafanyabiashara wenzao.

Mkutano huo utaanza saa 3:30 asubuhi na kurushwa mojakwamoja kupitia vyombo vya habari vya Redio, Televisheni na Youtube Channel ya Ikulu mawasiliano.

Wajumbe wote wanatakiwa kuwasili katika ukumbi wa Kikwete kuanzia saa 2:00 hadi saa 2:30 asubuhi.No comments