Breaking News

RAIS WA KONGO (DRC) AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA DKT. MAGUFULI JUNI 13, 2019.


Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi akikabidhiwa Ua la ishara ya Upendo na kumkaribisha Nchini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Rais Dkt. Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Rais Dkt. John  Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Tshisekedi wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi akikagua paredi maalumu aliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Magufuli kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Gwaride maalumu lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi na mwenyeji wake Rais Dkt.John  Magufuli wakitoa heshima katika hafla ya mapokezi iliyofanyika katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Rais Dkt.John  Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix  Tshisekedi wakati wakitazama kikundi cha ngoma wakati wa sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Rais Dkt.John  Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix  Tshisekedi wakati wakiwapungia mikono wananchin waliojitokeza katika sherehe za kumkaribisha Rais wa Kongo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.

Dkt.John  Magufuli akizungmza  na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ikulu kwaajili ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa.


Dkt. John  Magufuli akipokea zawadi kutoka kwa  Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC)  Felix  Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli.


Rais Dkt. John  Magufuli akimkabidhiu zawadi ya Picha ya Wanyama Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli.


Rais Dkt.John  Magufuli akiwa  Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix  Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya Mazungumzo na Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Mwaliko wa Rais Dkt.Magufuli.Rais Dkt.John  Magufuli akimtambulisha Rais wa awamu ya pili  Ali Hassani Mwinyi kwa Rais wa Jamhuri ya Kongo (DRC) Felix Antonio Tshisekedi Ikulu Jijini Dar es salaam katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam. Junin 13, 2019. PICHA NA IKULU

No comments