Breaking News

TAARIFA KWA WATANZANIA.Rais Dkt. John Magufuli, kesho tarehe 10 Juni, 2019 atawaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, Katibu tawala wa Mkoa wa Njombe, Charles Kichere na Lamishna Mkuu wa TRA Dkt. Edwine Mdehe.

Viongozi hao wataapishwa Ikulu Jijini Dar es salaam

Baada ya kuapishwa viongozi hao, Rais Magufuli atashuhudia tukio la kampuni ya Bharti Airtel International kutoa mchango wa Dola za Marekani Milioni 1 (sawa na shilingi bilioni 2 na Milion 270) ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo, na shilingi Bilioni 3 (ambazo zinatokana na malipo ya shilingi Bilioni 1 kila mwezi kwa Serikali) ikiwa ni makubaliano yaliyofanya kati ya Serikali na Bhart Airtel International kuhusu umiliki wa hisa za kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.

Matukio hayo yataanza saa 8:00 mchana na kurushwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari Radio, Televisheni, Mitandao na Youtube Chaneli ya Ikulu (Ikulu mawasiliano.)

No comments