Breaking News

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI ITATUE MGOGORO KATI YAO NA MWEKEZAJI.
Mkuu wa wilaya, Frank Mwaisumbe, Mkurugenzi wa halmashauri Jumaa mhina, mwenyekiti wa halmshauri Ken Moleiment na katibu wa CCM Juma Simba Gadafi.

Na Mashaka Mhando,Longido

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangallah ameombwa kuingilia kati na kutatua, mgogoro baina ya vijiji 23 na kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Green Miles Safari Ltd, ambao sasa imesababisha kukwama miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo mjini hapa, Diwani wa kata ya Kitumbeine  Thimoth Laizer alisema vijiji vyao ambavyo vinaidai kampuni hiyo kiasi cha sh 329 milioni, vimeshindwa kutekeleza miradi ya maendeleo, ikiwepo ujenzi wa shule na zahanati kutokana na kukosa fedha.

“vijiji vyetu vinategemea sana mapato ya utalii katika hiki kitalu ambacho alipewa Green Miles Sasa kwa zaidi ya mwaka sasa tunamgogoro na amegoma kulipa”alisema

Hata hivyo, Mkurugenzi wa kampuni ya Green Miles Safaris,Salim  Awadhi amekuwa akikanusha kudaiwa na vijiji hivyo na kueleza hana mkataba na vijiji.  

Mkazi wa kijiji chaa Lumbwa, Gerald Thadeo  alisema kwa takriban mwaka sasa, wamekuwa na mgogoro na kampuni hiyo na tayari kijiji chao kilipitisha azimio la kutofanyanayo kazi hasa kutokana na kushindwa kulipa vijiji.

“tunaomba Waziri aje kutatua kutatua mgogoro huu, kwani sisi kama wanavijiji sasa tunashindwa kufanya miradi kutokana na mwekezaji kutolipa kijiji”alisema

Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe alisema tayari suala hilo limefikishwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa maamuzi.

“Ni kweli miradi ya vijiji imesimama kwa kuwa wananchi walikuwa wanategemea fedha za kitalu cha uwindaji na kutokana na mgogoro huu hawamtaki tena mwekezaji huyu”alisema

Hata hivyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangallah tayari ameahidi kufika Longido kutatua mgogoro huu.

“bado tunamsubiri waziri, kwa upande wetu sisi kama serikali ya wilaya na hata mkoa tumekwishatoa maamuzi juu ya mwekezaji huyo ambaye amekuwa na matatizo na wananchi”alisema.

Waziri Kigwangallah hivi karibuni, aliahidi kuwa amepanga kutembelea wilaya ya Longido kutatua mgogoro huo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa kampuni ya Green Miles Safaris,Salim  Awadhi amekuwa akikanusha kudaiwa na vijiji hivyo na kueleza hana mkataba na vijiji.


No comments