Breaking News

WAONGOZA WATALII BORA NCHINI WAPEWA TUZO.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua hafla ya utoaji wa Tuzo za Waongoza Watalii nchini (Tanzania Tour Guides Awards 2019) kwa mwaka ,jijini Arusha.

Dkt. Kigwangalla akimkabidhi tuzo ya Mwongoza Watalii Bora upande wa Wanaume, Bw. Athuman Njiku, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo kwa waongoza watalii jijini Arusha

 Dkt. Kigwangalla akimkabidhi Tuzo ya mwongoza Watalii Bora wa muda mrefu Bi. Mary Mushi kwa kufanya kazi ya  kuongoza Watalii Mlima Kilimanjaro tangu mwaka 1979.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Peter Msigwa, kwa niaba ya Dkt. Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa mshindi wa Waongoza Watalii Bora wa muda mrefu kwa upande wa wanaume.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kemilembe Walter akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo kwa waongoza watalii kwa mwaka 2019, jijini Arusha

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kemilembe Walter akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa upande wa Wanawake mwaka 2019, Rehema Otalu wakati wa hafla  ya utoaji wa Tuzo hizo  jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Dkt.  Kigwangalla mmoja wa waashindi wa Tuzo ya waongoza Utalii Bora upande wa Utamaduni kwa mwaka 2019, jijini Arusha.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili, Utalii na Mbunge wa Nungwi - Zanzibar, Yusuf Haji Khamis kwa niaba ya Dkt. Kigwangalla, akimkabidhi Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora Bw. Gaudence Phesto kutoka kampuni ya Kuongoza watalii ya Leopord aliyeweka rekodi ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia muda wa saa 8.

Dkt. Kigwangalla (kushoto) akiwapongeza Washindi wa Tuzo ya Waongoza Watalii Bora kwa mwaka 2019 kwa upande wa Wapagazi Wanawake. Wa pili kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashindano ya Tuzo hizo Mozes Njowe kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA.

Majaji walioshiriki kuteua washindi wa Tuzo za waongoza Watalii kwa mwaka 2019 wakiwa katika  picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya utoaji wa tuzo hizo jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kemilembe Walter akimkabidhi  Alisya Sanga Tuzo ya Mwongoza Watalii Bora kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo kwa Mwongoza watalii Bora wanawake mwaka 2019, jijini Arusha.


No comments