Breaking News

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, KAMISHNA MKUU WA TRA WATUMBULIWA.Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 08 Juni, 2019 amemteua  Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Bashungwa anachukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kablaya uteuzi huo, Bashungwa alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Wakatihuohuo, Dkt. Magufuli amemteua Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mhede anachukua nafasi ya Charles Edward Kichere ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kabla ya uteuzi huo  Mhede alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara utafanywa baadaye.
Kufuatia uamuzi huo, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA  Charles Kichere ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
Kichere anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Erick Shitindi ambaye amestaafu.

No comments