Breaking News

MAJALIWA AHUDHURIA KONGAMANO LA WANAWAKE KIGOMA.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kufungua Kongamano la Wanawake (UWT) kitaifa, Julai 13, 2019.


 
Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa  Wanawake Tanzania  (UWT), Gaudencia Kabaka wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kufungua Kongamano la Wananwake  Kitaifa, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Dismas  Nzamba.
Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Kongamano la Wanawake  (UWT) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika  Julai 13, 2019.
              
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Wanawake  (UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019.

 
Majaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakitazama hot pot lililotengenezwa kwa mbao wakati alipohutubia katika Kongamano la Wanawake  kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Julai 13, 2019.

 
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Stella Ikupa akizungumza katika Kongamano la  Wanawake (UWT) lililohutubiwa na Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019.

No comments