Breaking News

MGALU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MAENDELEO YA USAMBAZAJI UMEME KIGOMA.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( katikati) akizungumza na mkazi wa kijiji cha Ruhita,wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, kabla ya kukata utepe kuwasha umeme katika nyumba yake ikiwa ni ishara ya kuwasha umeme katika kijiji hicho.


Makuruta wa kikosi cha 825KJ kambi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, hayupo pichani, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya hiyo.


Subira Mgalu Aakizungumza na makuruta wa kikosi cha 825KJ katika kambi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani Kigoma, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika wilaya hiyo. Subira Mgalu,( katikati) akimkabidhi kifaa cha umeme tayari( UMETA) mama mwenye ulemavu, Merania Katekwa, mkazi wa Kijiji cha Nyankoronko wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, ambaye hana uwezo wa kulipia gharama za kuunganisha umeme licha ya  nyumba yake kukidhi viwango  na kupitiwa na mradi wa usambazaji umeme vijijini.


Akina mama wa kijiji cha Shunga, Kasulu mkoani Kigoma, wakifurahi na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alipowaeleza kuwa umeme katika kijiji hicho utafika hivi karibu na tayari mkandarasi anaendelea na kazi ya kusimika nguzo.

No comments