Breaking News

SERIKALI YADHAMIRIA KUKUZA UTALII WA SOKWE NCHINI.Na. Aron Msigwa.

SERIKALI imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyoko wilayani Karagwe na Ibanda iliyoko Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa  na Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.

Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori 

No comments